top of page

KUTUHUSU

Chuo cha Kimataifa cha Biblia cha Misheni cha CRC ni kitengo cha mafunzo na maendeleo cha shirika la kimataifa la makanisa ya CRC ambayo hutoa masomo ili kusaidia ukuzaji wa watu binafsi ili waweze kufikia ukamilifu wa vipaji vyao jinsi Mungu alivyo kusudia.

 

Msingi wa Kibiblia – kukubali kwamba Biblia ndilo Neno halisi la Mungu. Kupitia usomaji wa Neno la Mungu kwa utaratibu washiriki watawekwa katika msingi kamili ya Maandiko na katika imani yao, na kutimiza himizo la mtume Paulo ya, “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” (2 Timotheo 2:15)

 

Utendaji wa Makini – kuandaa watu kwa huduma inayofaa. Tamanio letu si tu kupasha maarifa ya kinadharia, bali pia kutoa mafunzo ya utendaji katika vipengele vyote vya huduma. “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi ya kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.” (Waefeso 4:11-12)

 

 Unaobadili Tabia – ukuzaji wa wanafunzi thabiti ukitiliwa mkazo. Lengo letu ni kukuza wanaume na wanawake walio na tabio sawa na Kristo. Kwa hiyo tumejitolea kukuza sifa muhimu ya uwanafunzi na kutamani kuona ukuaji katika uthabiti na uaminifu, ishara bainifu za wafuasi wote wa Yesu. “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze baba yenu aliye mbinguni.” (Mathayo 5:16)

 

Msukumo wa Kiroho – kupasha maisha ya kiroho na nguvu. Lengo letu ni kuwaelekeza wanaume na wanawake jinsi ya kuenenda katika ukuu wa nguvu za Mungu zipitazo fahamu (kuwa wazi kwa kazi za Roho Mtakatifu), kukuza uhusiano Naye ni kipaumbele katika huduma yoyote. “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenuRoho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu.” (Matendo 1:8)

MAONO YETU

Kumfunza kiongozi Huduma ya Kikristo inayofaa katika Kanisa lake la nyumbani na ugenini kuwasilisha Injili kwa njia inayofaa.

Kila kozi katika Chuo cha Kimisheni cha CRC kimetungwa mahususi kuwafunza na kuwatayarisha wanaume na wanawake kwa kazi ya huduma kulingana na Waefeso 4:11-12.

Tunatambua kwamba huduma hutegemea kikamilifu karama za Mungu na lengo letu ni kutambua, kukuza na kuachilia karama ambazo Mungu ametoa.

bottom of page